Sunday, November 16, 2014

ZITTO KABWE AKUBALIANA NA KUPONGEZA UTAFITI WA TWAWEZA.

BOFYA HAPA CHINI KUONA MAAJABU YA LEO




WAKATI viongozi wa Ukawa wakipinga utafiti uliofanywa na TWAWEZA kwa madai ni mbinu chafu iliyotumika kwa maelekezo ya Kada mmoja wa Chama Cha Mapinduzi mwenye kiu ya kuwania
nafasi ya Urais mwaka 2015,Zitto Kabwe ameupongeza utafiti huo.

Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini  (CHADEMA),japo ana mgogoro na
chama chake hicho aliibuka
kukubaliana na kuupongeza utafiti huo,na kutoa ushauri tafiti hizo zifanyike kila baada ya miezi mitatu hadi hapo uchaguzi mkuu utapokapofanyika.

Kabwe ambaye katika utafiti wa kisiasa uliofanywa na Twaweza alipata asilimia sita kwa watu wanaofaa kuwania urais kupitia UKAWA, alisema tafiti za kura ya maoni(Opinion polls) ni muhimu katika demokrasia nchini.

Alisema kitendo kilichofanywa na TWAWEZA ni muhimu sana kwa viongozi wa kisiasa nchini hasa wenye dhamira ya kugombea madaraka katika uchaguzi mkuu ujao kujitathimini baada ya kutambua wanakubalika kiasi gani ndani ya jamii wanayoomba kuiongoza.

Aliwapongeza TWAWEZA kwa kufanya kazi nzuri huku akiwabeza wanaopinga tafiti hiyo,paspo kuleta majibu ya mbadala na kuwataka kuwa nao wanapaswa kuonyesha utafiti wao unavyosema kwa sababu utafiti unapingwa kwa utafiti na siyo kwa porojo.

KUONA VIDEO MPYA BOFYA HAPA CHINI